1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa nchi za karabu watoa ujumbe mkali kwa Israel

12 Novemba 2024

Viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu wameitaka Israel kuondoka katika maeneo yote ya Palestina inayoyakalia kimabavu kama sharti la awali la upatikanaji wa amani ya kudumu katika eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4muaY
Saudi-Arabien Riad 2024 |
Viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu wameitaka Israel kuondoka katika maeneo yote ya PalestinaPicha: Turkish Presidency/Murat Kula/Anadolu/picture alliance

Wito huo umetolewa katika mkutano wa kilele wa viongozi wa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu, uliofanyika mjini Riyadh Saudi Arabia, na kutoa fursa kwa viongozi wake kuzungumza kwa sauti moja juu ya machafuko yanayoendelea Mashariki ya Kati. 

Mwanamfalme wa Saudia bin Salman aitisha usitishwaji wa mapigano Gaza, Lebanon

Katika tamko lao la pamoja la kufunga mkutano wa kilele, viongozi wa mataifa hayo walisema amani ya kina katika eneo la Mashariki ya Kati, haiwezi kupatikana bila ya kukomeshwa ukaliaji wa kimabavu wa  Israel katika maeneo yote ya ardhi ya Wapalestina, kuambatana na mipaka ya 1967, ikiwemo Ukingo wa Magharibi, Jerusalem Mashariki, Ukanda wa Gaza na Milima ya Golan.