1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudia yaitisha usitishwaji wa mapigano Gaza, Lebanon

11 Novemba 2024

Mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, ametoa wito wa usitishaji mara moja wa vita katika Ukanda wa Gaza na Lebanon. Ameyasema hayo katika mkutano wa kilele unaofanyika Riyadh, Saudi Arabia.

https://p.dw.com/p/4mtFx
Mohammed bin Salman
Mohammed bin Salman ametoa wito wa usitishaji mara moja wa vita katika Ukanda wa Gaza na LebanonPicha: Johanna Geron/REUTERS

Bin Salman ametoa wito huo katika mkutano wa kilele wa pamoja wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu unaofanyika mjini Riyadh, Saudi Arabia.

Soma pia: Mataifa ya Kiarabu na Kiislamu yatoa wito wa kusitisha vita Gaza na Lebanon

Mkutano huo unatarajiwa kusisitiza kwa mara nyingine juu ya kuanzishwa kwa taifa la Palestina. Akifungua mkutano huo, Mwanamfalme Bin Salman, amesema.

"Tunatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutimiza wajibu wake wa kudumisha amani na usalama wa kimataifa kwa kukomesha mara moja mashambulizi ya Israeli dhidi ya ndugu zetu wa Palestina na Lebanon, na kuhakikisha kuwa Israeli inaheshimu mamlaka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kujiepusha na kushambulia maeneo yake."

Mikutano kama hiyo ilifanyika mwaka mmoja uliopita mjini Riyadh na Jeddah na kulaani vikali mashambulizi ya Israel huko Gaza.