1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa jumuiya ya madola wajadili mabadiliko ya hali ya hewa

24 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSku

Viongozi wa jumuiya ya madola, Commonwealth, wamejadiliana kuondoa tofauti zao juu ya tangazo la pamoja kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa hii leo.

Swala la Pakistan na kuchaguliwa kwa katibu mkuu mpya wa jumuiya hiyo yametuwama mada za mkutano wa kilele wa Commonwealth mjini Kampala Uganda.

Uingereza, India na Australia ambazo ni wanachama wa jumuiya ya madola, ni miongoni mwa nchi zinazotoa kiwango kikubwa cha gesi za viwandani.

Lakini nchi kama vile visiwa vya Maldives na Kiribati, ambavyo pia ni wanachama wa jumuiya hiyo, viko katika msitari wa mbele kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Jumuiya ya madola imemchagua balozi wa India nchini Uingereza, Kamlesh Sharma, kuwa katibu mkuu mpya.

Viongozi wa serikali wa jumuiya hiyo wamemchagua Sharma bila kupingwa kuchukua nafasi ya waziri wa zamani wa mashauri ya kigeni wa New Zealand, Don McKinnon, anayeondoka baada ya kushikilia wadhifa huo kwa miaka minane.

Wapinzani wakuu wa Sharma walikuwa waziri wa kigeni wa Malta, Micheal Frendo na Mohan Kaul, raia wa Uingereza.