1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Japan na Iran kukutana Septemba mjini New York

20 Agosti 2023

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida na rais wa Iran Ebrahim Raisi watakutana mjini New York mwezi Septemba kujadili kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran miongoni mwa mambo mengine muhimu.

https://p.dw.com/p/4VNTC
Irans Präsident Ebrahim Raisi besucht Simbabwe
Picha: Iran's Presidency/Mohammad Javad Ostad/WANA/REUTERS

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida na rais wa Iran Ebrahim Raisi watakutana mjini New York mwezi Septemba kujadili kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran miongoni mwa mambo mengine muhimu. 

Shirika la habari la Japan Kyodo limesema Iran inanuia kuimarisha mahusiano yake na Japan ili kukwepa kubaguliwa kimataifa kufuatia mazungumzo ya Iran na Marekani pamoja na Ulaya juu ya mpango wa nyuklia wa Iran kukwama. 

Iran yakanusha kuongeza kurutubisha madini ya urani

Hapajakuwa na tamko lolote kutoka kwa wizara ya mambo ya nje ya Japan kuhusu mkutano huo.  

Mwezi Septemba mwaka jana Kishida na rais walikutana katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  mjini New York.