1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa G20 wanakutana Brazil kujadili mazingira

19 Novemba 2024

Viongozi wa kundi la G20 wametangaza azimio la mwisho, katika siku ya kwanza ya mkutano wao wa kilele jana Jumatatu, ambalo hata hivyo, lilijumuisha taarifa iliyogusia migogoro katika Mashariki ya Kati na Ukraine.

https://p.dw.com/p/4n90g
G20-Gipfel | Brasilien, Rio de Janeiro | Macron und Biden im Gespräch bei einer Arbeitssitzung
Emmanuel Macron rais wa Ufaransa na Joe Biden rais wa Marekani wakizungumza wakati wa kikao cha kwanza cha kazi kama sehemu ya Mkutano wa G20 2024 huko Museu de Arte Moderna Novemba 18, 2024, Brazil.Picha: Buda Mendes/Getty Images

Brazil ambayo ni mwenyeji wa mkutano huo iliandaa ajenda iliyoorodhesha masuala ya kipaumbele ambayo ni pamoja na kukabiliana na njaa na mabadiliko ya tabia nchi sambamba na juhudi za kuyafanyia mageuzi mashirika ya Kimataifa. Hii leo Jumanne viongozi wanaokutana watajadili suala la maendeleo endelevu pamoja na mpango wa kuingia kwenye matumizi ya nishati safi na kuondokana na nishati zinazochafua mazingira. Viongozi hao wanalenga kuongeza hatua ya kupatikana makubaliano ya ufanisi ya kushughulikia ongezeko la joto duniani katika mkutano wa mazingira wa Umoja wa Mataifa unaoendelea Azerbaijan.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW