1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Umoja wa ulaya vyaanza kuwajibika Mali

2 Aprili 2013

Wanajeshi wa Umoja wa Ulaya wanaanza kuwapatia mafunzo wanajeshi wa Mali katika wakati ambapo opereshini za kijeshi zinazoongozwa na Ufaransa zinaendelea katika mji wa kaskazini wa Timbuktu .

https://p.dw.com/p/1883O
Waziri wa ulinziThomas de Maiziere akiwatembelea wanajeshi wa Ujerumani nchini MaliPicha: Reuters

Kouli Koro ni mji unaokutikana umbali wa saa moja kwa gari kutoka mji mkuu wa Mali-Bamako.Huko ndiko wanajeshi wa Umoja wa Ulaya walikopiga kambi yao-mbali kabisa na uwanja wa mapigano,kaskazini ya Mali.Miongoni mwa wanajeshi hao wa Umoja wa ulaya wanakutikana matabibu 40 wa kutoka jeshi la Ujerumani Bundeswehr na waalimu 40 watakaosaidia kuwapatia mafunzo ya kijeshi makuruti wa Mali.Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Thomas de Maizière alipowatembelea wanajeshi wa Ujerumani alitoa wito kwa mara nyengine tena wa kutolewa misaada kupambana dhidi ya wafuasi wa itikadi kali ya dini ya kiislam kaskazini ya Mali:

"Ni kitisho kwa eneo lote la Sahel.Na Mali haiko mbali na bahari ya kati.Kwa hivyo ni kwa masilahi ya Ulaya pia kuhakikisha ugaidi hauenei nchini Mali."Amesema waziri wa ulinzi wa serikali kuu ya Ujerumani.

Jukumu la Wanajeshi wa Umoja wa Ulaya sio kupigana

Umoja wa Ulaya unapanga kuwapatia mafunzo wanajeshi 4000 wa Mali-wanajeshi wa Ujerumani wanawashughulikia mafundi.Dhahir ni kwamba tume ya Umoja wa Ulaya haitoshiriki katika mapigano na wakati wao umewekewa kikomo pia.Hata hivyo Umoja wa ulaya umejiachia uwezekano wa kurefusha muda ikihitajika:Mpango wa Umoja wa Ulaya umepangwa kuendelea kwa muda wa miezi 15.Viongozi wa serikali ya Mali wamedhamiria kuona muda huo haupindukii.Suala lakini ni kama utatosha?Itategemea kama ufanisi utakaopatikana utakuwa wa kutia moyo."

Serikali ya Mali inapendelea kuona juhudi za Umoja wa Ulaya zikileta tija haraka.Waziri wa ulinzi wa Mali Yamoussa Camara anasema anataraji vikosi vyao vya usalama vitaweza haraka na kwa ufanisi kuyakomboa haraka maeneo pamoja na kudhamini usalama na kushiriki katika meza ya mazungumzo.

Juhudi za amani ziendelezwe

Umoja wa ulaya ndio unaoshinikitza mazungumzo yafanyike pamoja na makundi ya upande wa upinzani.Waziri wa ulinzi wa serikali kuu ya Ujerumani anasema mazungumzo hayo ni sehemu ya utaratibu wa kuleta suluhu ambao siku za mbele utayajumuisha pia makundi ya kaskazini ya Mali.Utaratibu huo ni pamoja na kuitishwa uchaguzi Julai mwaka huu.

Mwandishi:Mänz,Alex/DW-TV/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman