1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis yuko salama hospitalini licha ya maambukizi

30 Machi 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis amekuwa na usiku wa kwanza mtulivu hospitalini baada ya kulazwa akiwa na maambukizi katika mfumo wa kupumua.

https://p.dw.com/p/4PUg0
Papst Franziskus
Picha: Stefano Spaziani/picture alliance

Afisa mmoja wa Vatican amesema taarifa zaidi za kimatibabu zitatolewa baadae leo. Francis alipelekwa jana mchana katika hospitali ya Gemelli mjini Rome kwa ajili ya vipimo baada ya kukumbwa na matatizo ya kupumua katika siku za karibuni.

Papa Francis mwenye umri wa miaka 86, ambaye wakati akiwa kijana, sehemu ya mapafu yake iliondolewa, hana maambukizi ya UVIKO-19 lakini ataendelea kuwa hospitalini kwa siku kadhaa kwa matibabu.

Papa Francis alazwa hospitali kwa changamoto ya upumuaji

Kiongozi huyo wa Kikatoliki anatarajiwa kuongoza maadhimisho ya Jumapili ya Matawi mwishoni mwa wiki hii, na haijajulikana kama hali yake ya kimatibabu itaathiri ratiba ya Wiki Takatifu itakayoishia Jumapili ya Pasaka mnamo Aprili 9.