Papa Francis alazwa hospitali kwa changamoto ya upumuaji
30 Machi 2023Matangazo
Msemaji wa Vatican Matteo Bruni amesema, katika siku za karibuni Papa Fracis amelalamika juu ya changamoto ya kupumua, lakini akisisitiza si Corona.Chanzo kutoka Vatican kimethibitisha kwamba shughuli za Papa kwa siku ya Alhamis zilisitishwa,wakati huu ambao kumegubikwa shughuli nyingi kwa Papa kuelekea sikukuu ya Pasaka.
Licha ya uzee na changamoto za kiafya Papa Francis ameendelea kusafiri, ambapo mapema mwaka huu alifanya ziara nchini Jamhuri ya kidemocrasia ya Kongo na Sudan Kusini na kulakiwa na mamia kwa maelfu ya waumini,viongozi na wakuu wa nchi hizo.
Mwezi ujao, anatarajiwa kutembelea Hungary na kukutana na Waziri Mkuu Viktor Orban.