1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utawala wa kijeshi Guinea utarejesha utawala wa kiraia?

25 Aprili 2022

Utawala wa kijeshi nchini Guinea umeonyesha dalili za kuvunja ahadi yake ya kuanza mpango mpya wa kuirejesha nchi hiyo katika utawala wa kiraia na kujiondoa kwenye vikwazo na ECOWAS

https://p.dw.com/p/4AQ2P
Burkina Faso Militärseelsorger
Picha: Sophie Garcia/AP/picture alliance

Hakukuwepo na tangazo kutoka utawala wa kijeshi wa Burkina Faso ambao pia walikuwa wanakabiliwa na muda wa mwisho wa leo Jumatatu wa kuwasilisha mpango unaokubalika wa kurudisha madaraka kwa raia baada ya jeshi kuchukua uongozi wa taifa kupitia mapinduzi ya mwezi Januari yaliyomuondoa madarakani Rais Rock Kabore.

Afrika Magharibi imeshuhudia mapinduzi mawili ya kijeshi tangu Agosti mwaka 2020, la kwanza nchini Guinea na lengine nchini Burkina Faso.

Viongozi wa jumuiya ya ECOWAS waliuambia utawala wa kijeshi wa Guinea na Burkina Faso kwamba wana muda wa mwisho wa hadi Aprili 25 kufafanua jinsi watakavyorudisha madaraka kwa umma, la sivyo watakabiliwa na vikwazo.

Soma zaidi:Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi wakaa kimya kimya na makundi ya wanamgambo

Alipoulizwa juu ya muda wa mwisho wa kuwasilisha mapendekezo ya jinsi ya kurudisha utawala wa kiraia, msemaji wa serikali ya Guinea alisema: "Uhalisia wa Guinea utashinda masharti yote na vikwazo vyovyote.”

 

ECOWAS imesalia kimya hata baada ya terehe ya uchaguzi kuvuka

Jumuiya wa ECOWAS haikujibu ombi la shirika la habari la Reuters kuhusu namna na muda wa vikwazo dhidi ya Burkina Fasona Guinea iwapo nchi hizo mbili zitakosa kutekeleza masharti baada ya muda wa mwisho kukamilika Aprili 25.

Ghana Accra | Economic Community of West African States | ECOWAS
Viongozi wa ECOWAS wakiwa katika kikao kaziPicha: IVORY COAST PRESIDENTIAL PRESS SERVICE/REUTERS

Mnamo siku ya Jumapili, msemaji wa utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso Lionel Bilgo alisema kurejesha amani na usalama ni sharti muhimu kabla ya kurejeshwa kwa utawala wa kikatiba.

Soma zaidi:Burkina Faso yapata rais mpya wa mpito

Hata hivyo, Baraza la kitaifa la mpito la Guinea bado halijatangaza tarehe ya uchaguzi baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais Alpha Conde mnamo mwezi Septemba.

Jumuiya ya ECOWAS tayari imeiwekea Mali vikwazo, wakati mkuu aliyeongoza mapinduzi dhidi ya serikali mnamo Agosti 2020 na baadaye akampiga kumborais wa mpito mwezi Mei, 2021.

Ujerumani kuisaidia Burkina Faso kupambana na uasi