Ushirikiano baina ya wanaharakati wa mazingira wa Ujerumani na Tanzania
12 Septemba 2008Matangazo
Leo karibu na mitambo ya umeme inayopangwa kujengwa na ambayo itatokana na nishati ya makaa katika eneo la Staudinger na Jänschwalde hapa Ujerumani, kutafanywa maandamano kupinga kujengwa mitambo hiyo. Kama wazungumzaji katika maandamano hayo watakuweko wanaharakati wa kulinda mazingira kutoka Tanzania, Bolivia, India, Kirgizistan na Visiwa vya Fiji. Wao wamealikwa na wanaharakati wa mazingira wenziwao wa hapa Ujerumani. Kwani uchafuzi wa mazingira katika nchi tajiri za viwanda unaleta athari kwa nchi maskini zinazoendelea, hivyo kumeonelewa umuhimu wa kuowanisha harakati za kulinda mazingira duniani kote.
Kutoka Tanzania atashiriki katika maandamano ya leo Grace Mketto wa kutoka Dodoma.