Urusi yakanusha UN kuwahamisha watoto wa Ukraine
23 Januari 2024Urusi imesisitiza katika Umoja wa Mataifa kwamba haijawaondoa kwa nguvu watoto wowote wa Ukraine kuwaleta nchini mwake tangu ilipomvamia jirani yake Februari mwaka 2022, kauli inayopingana na madai ya Kiev na mashirika yasio ya kiserikali.
Urusi iliyasema hayo baada ya kuulizwa na kamati ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za watoto, kutoa idadi kamili ya watoto waliopelekwa Urusi kutoka Ukraine au katika maeneo yanayodhibitiwa na Urusi nchini Ukraine tangu uvamizi ulipoanza.
Soma pia: Maelfu ya watoto wa Ukraine wamepelekwa Belarus
Ukraine inakadiria watoto 20,000 wa nchi hiyo wamepelekwa kwa nguvu nchini Urusi.
Mwaka 2023 Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC ilitoa waranti ya kukamatwa Rais Vladmir Putin kwa uhalifu wa kivita ikimtuhumu kuwapeleka Urusi kinyume cha sheria watoto wanaotoka Ukraine.