Urusi yakanusha kupeleka wakimbizi Finland
20 Novemba 2023Finland ilifunga mipaka yake minne na Urusi wiki iliyopita kufuatia kuongezeka kwa idadi ya waomba hifadhi, na kuituhumu Moscow kwamba inajaribu kuiyumbisha nchi hiyo kufuatia hatua yake ya kujiunga na Jumuiya ya kujihami NATO.
Msemaji wa Ikulu ya Urusi Dmitry Peskov aliwaambia waandishi habari kuwa Urusi haitokubali madai kama hayo, akisema vivuko vya mpakani vinatumiwa na wale walio na haki ya kufanya hivyo.
Soma pia:Urusi imefanya mashambulizi dhidi ya Ukraine baada ya wiki kadhaa ya kusimamisha mapigano
Alexander Grushko Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi amesema uamuzi wa Finland kufunga mipaka yake unakinzana na masilahi ya taifa hilo.
Mahusiano ya mataifa hayo mawili yameingia doa tangu Urusi ilioanzisha uvamizi wake nchini Ukraine mwaka uliyopita.