Urusi: Uingereza kupeleka kikosi Ukraine ni kutangaza vita
12 Januari 2024Medvedev ambaye kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi ametoa matamshi hayo akijibu ziara ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak nchini Ukraine, ambapo ametangaza kuongeza ufadhili wa kijeshi kwa kuisaidia Ukraine kununua ndege mpya za kijeshi.
Medvedev ameandika leo katika mtandao wa kijamii wa Telegram kwamba ana matumaini maadui zao, Uingereza aliyosema imejaa "majivuno" inaelewa kuwa kupeleka kikosi rasmi cha kijeshi nchini Ukraine itakuwa tangazo la vita dhidi ya Urusi.
Soma pia:Zelenskiy asema usitishaji mapigano Ukraine utainufaisha tu Urusi
Pia ameyauliza mataifa ya Magharibi yatajisikia vipi iwapo ujumbe wa Sunak utashambuliwa katikati ya Kiev, jambo ambalo amesema limetokea hivi karibuni kwa raia wa Urusi kwenye mji wa Belgorod.