Guterres ataka suluhu ya Mataifa mawili Israel na Palestina
21 Januari 2024Guterres alisema jana Jumamosi kwamba haki ya wapalestina kuwa na taifa lao ni lazima itambuliwe na kila mmoja.
Akizungumza mjini Kampala katika mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya nchi zisizofungamana na upande wowote, Guterres alisema hatua ya kukataa kutambuwa haki hiyo kwa watu wa palestina haitokubalika.
Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kukataliwa suluhu ya mataifa mawili kunaendeleza mgogoro uliopo ambao umekuwa tishio kwa usalama na amani ya dunia na kuchangia ubaguzi na kuendeleza misimamo mikali kila sehemu.
Nchi za kiarabu na Ulaya zapigia debe suluhisho la mataifa mawili mzozo wa Mashariki ya Kati
Amerejelea pia wito wake wa kutaka kusimamishwa kwa mapigano kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Nentanyahu ameendelea kukataa mpango wa suluhu ya Mataifa mawili katika mgogoro huo wa Israel na Palestina.