UN yatoa wito kwa makampuni kutoa fedha ili kuziokoa bahari
28 Juni 2022Takriban watu 7,000 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano unaohusu bahari,ulioandaliwa na Umoja wa mataifa,huko mji wa Lisbon nchini Ureno. Mkutano huo utahusisha wakuu wa nchi, wanasayansi na mashirika yasiyo ya kiserikali, ili kutathmini maendeleo katika kutekeleza agizo la kulinda maisha ya majini.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumzia hali iliyopo sasa kuhusu bahari duniani amesema "inasikitisha, tunaiona bahari ni kitu cha kawaida, na leo tunakabiliana na kile ninachoweza kukiita "dharura ya bahari".
Soma pia: Mkutano wa kilele wa kunusuru bahari wafanyika Ufaransa
"Ni lazima tuibadilishe hali hiyo. Ongezeko la joto duniani linasababisha viwango vya joto baharini kuongezeka kwa kiasi kikubwa na kusababisha dhoruba za mara kwa mara. Vina vya maji ya bahari vinaongezeka. Mataifa ya visiwa yanakabiliwa na mafuriko kama ilivyo pia kwa miji mikubwa ya pwani duniani.''
Guterres aliongezea kuwa, kunahitajika biashara ya mfano, ambayo itasaidia bahari kuzalisha chakula na nishati mbadala."Hiyo inahitaji viwango vipya vya ufadhili wa muda mrefu,"
Taka za plastiki, kikwazo kwa viumbe wa majini
Bahari ni karibu asilimia 70 ya uso wa sayari, ambapo inazalisha asilimia 50 ya oksijeni na kunyonya asilimia 25 ya kaboni dioksidi
Lakini mabadiliko ya hali ya hewa yanapelekea joto la bahari kufika kiwango cha juu na kutengeneza tindikali zaidi. Aliongezea kuwa tani milioni nane za taka za plastiki huingia baharini kila mwaka."Bila hatua kali, taka za plastiki zinaweza kuzidi samaki wote samaki baharini ifikapo mwaka 2050,"
Mnamo mwezi Machi, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zilishindwa kukubaliana juu ya mkataba wa kulinda bahari kuu dhidi ya unyonyaji.
Soma pia: Dalili njema zaibuka kwenye mkutano wa Mazingira wa Durban
Peter Thomson, Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya bahari, aliambia shirika la habari la Reuters kuwa, alikuwa na imani kwamba makubaliano yatafikiwa mwaka huu.
Taka za palstiki zilizopatikana ndani ya samaki kwenye kina kirefu cha bahari,zinakadiriwa kuua zaidi ya mamilioni ya ndege wa baharini na pia viumbe wa majini zaidi ya millioni kila mwaka.
Suluhisho ni kufikia viwango vya kimataifa vya kuchakata na uzalishaji wa plastiki. Uvuvi wa kimataifa pia utaangaziwa katika mkutano huo wa siku tano, unaohusu bahari,ulioandaliwa na Umoja wa mataifa.
"Theluthi moja ya hifadhi ya samaki mwitu wamevuliwa kupita kiasi na chini ya asilimia 10 ya bahari inalindwa," Kathryn Matthews, mwanasayansi mkuu wa shirika lisilo la kiserikali lialoshughulikia masuala ya bahari yenye makao yake nchini Marekani ya Oceana, aliiambia shirika la habari la AFP.
"Meli na za uvuvi haramu zinafanya kazi bila kuthibitiwa kwenye maji mengi ya pwani na bahari kuu."Mkutano huo pia utajadili jinsi ya kusitishwa kwa uchimbaji wa madini katika kina kirefu cha bahari.Wanasayansi wanasema mifumo ikolojia ya chini ya bahari ni dhaifu na inaweza kuchukua miongo kadhaa au zaidi ili kutengamaa..
(Reuters)