1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yataka hatua za haraka kukabiliana na upungufu wa maji

Angela Mdungu
25 Machi 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema jamii inahitaji kuchukua hatua sasa kukabiliana na upungufu wa maji safi

https://p.dw.com/p/4PEjS
USA, New York | UN-Wasserkonferenz
Picha: Koen van Weel/ANP/picture alliance

Guterres, ameyasema hayo jana Ijumaa 24.03.2023 katika siku ya mwisho ya mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maji uliofanyika kwa siku tatu jijini New York nchini Marekani.

Soma zaidi:UN: Uhaba wa maji watishia mzozo wa kimataifa

Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa ni muhimu kuanzisha njia mpya za mifumo kupunguza matumizi ya maji yasiyo endelevu katika uzalishaji chakula na kilimo.

Katibu mkuu wa UN Antonio Guterres akihutubia mkutano wa maji, New York
Katibu mkuu wa UN Antonio Guterres akihutubia mkutano wa maji, New YorkPicha: Koen van Weel/ANP/picture alliance

Mkutano huo umefanyika kwa mara ya kwanza baada ya karibu nusu muongo na kuibua matumaini ya kuchochea kasi ya kisiasa, katika kuimarisha hatua za kukabiliana na tatizo sugu la maji duniani.

Chanzo: DPAE