1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Watu wavunja maghala na kuchukua misaada Gaza

Hawa Bihoga
29 Oktoba 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi na Misaada kwa Wakimbizi wa Palestina UNRWA limesema maelfu ya watu wamevunja maghala na vituo vya usambazaji wa misaada katika Ukanda wa Gaza, na kuchukua vyakula.

https://p.dw.com/p/4YAK7
Mkurugenzi wa UNRWA Thomas White
Mkurugenzi wa UNRWA Thomas WhitePicha: Mustafa Hassona/AA/picture alliance

Thomas White, Mkurugenzi wa UNRWA amesema ishara hiyo inatia wasiwasi kwamba utaratibu wa kawaida wa kiraia utavurugwa baada ya wiki tatu za vita na mzingiro kwa Gaza na kuongeza kwamba watu wanahofu, wamechanganyikiwa na pia wamekata tamaa.

Hali ya usambazaji bidhaa Gaza ilikuwa ni mbaya hata kabla ya vita kuanza na imezidi kuvurugika kutokana na mzingiro na kusambaratika kwa watu. Takriban malori 80 yenye bidhaa yaliingia katika Ukanda wa Gaza kutoka Misri kupitia kivuko cha mpaka cha Rafah tangu vita vilipozuka wiki tatu zilizopita.

Soma pia:Mkuu wa Haki za Binadamu aonya kuhusu operesheni ya Israel huko Gaza

Jana Jumamosi hakuna msafara ulioweza kuingia Gaza kutokana na kuharibika kwa miundombinu ya mawasiliano.