SiasaIsrael
Hamas yaapa kujibu mashambulizi ya Israel Ukanda wa Gaza
28 Oktoba 2023Matangazo
Kundi hilo la wanamgambo wa Kipalestina linalotawala Ukanda wa Gaza limearifu kwamba wapiganaji wake tayari wanakabiliana na vikosi vya Israel kwenye maeneo ya mpaka, kufuatia tangazo la Israel kuwa litazidisha mashambulizi yake ndani ya Gaza.
Kulingana na wizara ya afya ya Gaza, mashambulizi hayo ya Israel yamewauwa zaidi ya watu 7,000 kwenye ukanda huo tangu yalipoanza mwanzoni mwa mwezi huu kujibu shambulizi baya kabisa la kundi la Hamas la mnamo Oktoba 7.
Siku hiyo wanamgambo wa Hamas waliingia Israel na kufanya mauaji ya watu 1,400 na kuwachukua mateka mamia wengine. Israel, Marekani na mataifa mengine kadhaa ya magharibi yameliorodhesha kundi la Hamas kuwa la kigaidi.