UN: Watu nusu milioni wakikimbia mapigano Kongo
24 Novemba 2023Matangazo
Shirika hilo limesema watu 450,000 wameyakimbia mapigano huku 200,000 wakiwa ni wakimbizi wa ndani ambao kwa sasa wanakabiliwa na uhaba wa misaada ya kibinaadamu, na kwamba kumekuwa kukishuhudiwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binaadamu ikiwa ni pamoja na ubakaji.
Soma pia:M23 wakiteka tena kijiji cha Kishishe mashariki mwa Kongo
UNHCR imesema hali inazidi kuzorota katika mkoa wa Kivu Kaskazini unaopakana na mataifa ya Uganda na Rwanda na kwamba eneo hilo limekumbwa na mgogoro kwa muda mrefu. Vikosi vya serikali vinajaribu kuchukua udhibiti wa eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa rasilimali.