1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMarekani

U.N: Mkutano kuhusu maji kuibua matumaini mapya

25 Machi 2023

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa mwito wa dharura kwa ulimwengu kuviboresha na kulinda vyanzo vya maji.

https://p.dw.com/p/4PEUi
Global Ideas Trockengebiete Artenvielfalt
Picha: Urs Schaffner

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa mwito huo ili kuepusha migogoro na kuhakikisha ustawi wa siku zijazo duniani.

Guterres amesema hayo wakati wa ufungaji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maji uliofanyika kwa mara ya kwanza baada ya karibu nusu muongo na kuibua matumaini ya kuchochea kasi ya kisiasa katika kuimarisha hatua za kukabiliana na tatizo sugu la maji kote ulimwenguni.

Hakujakuwa na makubaliano yanayofungamana kimataifa ya maji kama ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi yaliyofikiwa mjini Paris mwaka 2015 ama hata mpango kazi kama uliofikiwa Montreal mwaka uliopita, licha ya maonyo juu ya kitisho kinachowakabili wanadamu iwapo maji hayatasimamiwa vizuri.

Soma Zaidi: UN yaonya kuhusu matumizi mabaya ya maji