1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umuhimu wa China na Marekani katika ulinzi wa mazingira

3 Desemba 2009

China na Marekani ni wazalishaji wakubwa kabisa wa gesi zinazochafua mazingira.Ikiwa nchi hizo hazitokuwa tayari kutoa ahadi sahihi basi hata nchi nyingi zingine vile vile zitakuwa na msimamo kama huo.

https://p.dw.com/p/KpVX
Der Chef der Umweltbehörde der Vereinten Nationen (UNEP), Achim Steiner, aufgenommen am Donnerstag (15.03.2007) auf einer Pressekonferenz anlässlich des G8 Umweltministertreffens in Berlin. Foto: Tim Brakemeier dpa/lbn +++(c) dpa - Report+++
Achim Steiner, Mkuu wa Mipango ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa.Picha: picture-alliance / dpa

Ni dhahiri kuwa Marekani na China zina umuhimu mkubwa kwa matokeo ya mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa. Kwa maoni ya Martin Kaiser anaeongoza tume ya walinzi wa mazingira "Greenpeace" katika mkutano ujao wa kimataifa mjini Copenhagen, mkataba wa mazingira hautokuwa na uzito bila ya Marekani na China. Nchi hizo mbili zinahitajiwa ili mkataba mpya utakaochukua nafasi ya Itifaki ya Kyoto uweze kuwa chombo cha kimataifa cha kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

Lakini ishara zilizochomoka hivi karibuni katika mkutano mkuu wa APEC nchini Singapore zimevunja moyo. Sasa hakuna matumaini kuwa Rais wa Marekani Barack Obama ataungwa mkono na bunge lake kutoa ahadi sahihi kuhusu mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa.Na China nayo, katika suala la kupunguza uzalishaji wa gesi zinazochafua mazingira, inatanguliza mbele ukuaji wa uchumi wake. Licha ya hayo yote, Mkuu wa Mipango ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa, Achim Steiner anaamini kuwa misimamo ya nchi hizo mbili isikosolewe sana na kuongezea hivi:

"Ninadhani kuwa China na Marekani katika majadiliano ya mazingira zinatahminiwa zaidi kwa wakati wake uliopita badala ya kutia maanani mitazamo ya siku zijazo . Kwa bahati mbaya hata wanasiasa hufanya hivyo hivyo."

Wakati huo huo Steiner anasema, cha kuchekesha ni kwamba Marekani na China zitanufaika ikiwa zitapunguza gesi zinachofua hewa, kwani hatimae nchi hizo mbili zitafaidika kiuchumi na kiteknolijia.

Juu ya hivyo misimamo inayochukuliwa na mataifa hayo mawili kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa haionyeshi sura halisi ya nchini mwao. Kwani nchini Marekani jamii nyingi zimepiga fora katika ulinzi wa mazingira kulinganishwa na serikali kuu mjini Washington. Kwa mfano licha ya serikali iliyopita ya Bush kukataa kutia saini yake katika Itifaki ya Kyoto, zaidi ya jamii 300 zinatekeleza malengo ya itifaki hiyo. Na hata Gavana wa California Arnlod Scwarzenneger kwa wingi wa chama cha Demokrats katika serikali ya jimbo lake, ametoa amri ya kupunguza uzalishaji wa gesi zinazochafua mazingira kwa asilimia 20 ifikapo mwaka 2025.

China nayo imepiga fora kutengeneza umeme kwa kutumia miale ya jua na nguvu za upepo. Huo ni mwanzo lakini jitahada hizo bado hazitoshi. Kwa hivyo kwenye mkutano wa Copenhagen madola hayo mawili makuu yanapaswa kutoa ahadi sahihi.

Mwandishi:H.Jeppesen/ZPR/P.Martin

Mhariri: Hamidou,Oumilkher