Umoja wa mataifa, New York. Katibu mkuu afisu makubaliano ya umoja wa Ulaya kuhusu mazingira
10 Machi 2007.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amesifu makubaliano ya kihistoria ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyofikiwa na viongozi wa umoja wa Ulaya mjini Brussels jana Ijumaa, akisema kuwa yanaleta matumaini ya kuboresha ushirikiano wa kimataifa katika kupunguza utoaji wa gesi zinazoharibu mazingira.
Msemaji wa katibu mkuu Michele Montas amesema katika taarifa kuwa , katibu mkuu ameukaribisha uamuzi wa viongozi wa umoja wa Ulaya wa kuweka malengo ya kuwa na matumizi mazuri ya nishati na matumizi ya nishati endelevu.
Wakichukua nafasi ya harakati za mapambano dhidi ya ujoto duniani , viongozi wa umoja wa Ulaya walikubaliana kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa kutumia mitambo inayotumia zaidi upepo kuzalisha nishati, nguvu za jua pamoja na balbu zenye kutumia umeme mdogo, na kuahidi kuwa asilimia tano ya nishati ya mataifa hayo itatokana na nishati endelevu ifikapo mwaka 2020.