Ukeketaji ni ukiukaji wa haki za binadamu na kosa la jinai katika baadhi ya nchi. Shirika la Afya Duniani linakadiria kwamba kati ya wasichana na wanawake milioni 100 na 140 wamefanyiwa ukeketaji. Wengi wa wanawake na wasichana hawa wanaishi katika nchi 28 za Afrika , chache katika Mashariki ya Kati na Asia, na kati ya jumuiya za wahamiaji katika Ulaya.