1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMamlaka ya Palestina

Ujerumani yapeleka misaada katika ukanda wa Gaza

20 Desemba 2023

Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imedai inafanya kila liwezekanalo "kutuliza" hali katika ukanda wa Gaza huku ikitangaza kupeleka mahema makubwa 120 katika eneo la Al-Arish nchini Misri.

https://p.dw.com/p/4aMtT
Wapalestina wakikimbilia misaada ya kibinadamu ukanda wa Gaza
Wapalestina wakikimbilia misaada ya kibinadamu ukanda wa GazaPicha: Fatima Shbair/AP Photo

Katika vidio iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, mjumbe maalum wa Ujerumani kuhusu masuala ya kibinadamu katika eneo la Mashariki ya Kati Deike Potzel, ametangaza kuwa ndege ya kijeshi ya Ujerumani imepeleka mahema ili kuwasaidia wakaazi wa Gaza.

Potzel ameongeza kuwa, ndege mbili nyingine zitapeleka magodoro 10,000, vitanda 5,000 na idadi isiojulikana ya mitungi ya kuhifadhia maji.

Mjumbe huyo maalum wa Ujerumani kuhusu masuala ya kibinadamu katika eneo la Mashariki ya Kati ameeleza kuwa Ujerumani imeongeza kwa kiasi kikubwa misaada na itatoa kiasi dola milioni 220 kwa ajili ya kuyasaidia mashirika mbalimbali ya kibinadamu.

Amesema "Ujerumani inataka kusaidia watu wa Gaza," na ameapa kuwa serikali ya mjini Berlin inafuatilia kikamilifu sera zake za nje katika ngazi zote ili kupunguza mateso kwa wakaazi wa Gaza.