1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Svenja Schulze afanya ziara Mashariki ya Kati

19 Desemba 2023

Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani, Svenja Schulze, ameanza kile kinachoitwa "ziara ya kutafuta ukweli" nchini Israel na kwenye maeneo ya Wapalestina

https://p.dw.com/p/4aKeL
Lateinamerika und Karibik | Entwicklungsministerin Svenja Schulze
Picha: Janine Schmitz/photothek/IMAGO

Waziri Schulze anatarajiwa kukutana na wawakilishi wa asasi ya kiraia ya nchini Israel pamoja na watu walioathirika kutokana na shambulio la Hamas la tarehe 7 mwezi Oktoba.  

Waziri huyo wa Ujerumani pia atafanya mazungumzo na wakaazi wa mji wa Kibbutz ulio karibu na mpaka wa Gaza.

Israel yaendeleza mashambulizi Gaza huku miito ya usitishwaji vita ikitolewa

Baadaye, Waziri Schulze atakutana na Waziri Mkuu wa Palestina, Mohammad Shtayyeh, na pia atatembelea kambi ya wakimbizi ya Al-Amari iliyopo kwenye Ukingo wa Magharibi, ambako atakutana na wawakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi kwa Wapalestina (UNRWA).