SiasaUkraine
NATO yaikumbusha Ujerumani kuongeza mchango wa ulinzi
17 Septemba 2023Matangazo
Kwenye mahojiano na shirika la habari la Ujerumani Funke, katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amekumbushia enzi ya Vita Baridi wakati makansela Konrad Adenauer na Willy Brandt walipochangia asilimia tatu hadi nne ya pato la taifa kwenye bajeti ya ulinzi.
Amesisitiza kama hilo liliwezekana wakati huo, ni lazima lifanyike tena sasa.
Muda mfupi baada ya Urusi kuivamia Ukraine, kansela wa Ujerumani Olaf Scholz aliahidi yuro bilioni 100 ya bajeti ya mwaka 2022 ya matumizi ya kijeshi na pia aliahidi kufikisha asilimia mbili ya pato la ndani la Taifa kwenye matumizi ya ulinzi ya NATO.