Ujerumani haitoweka sheria kwa lengo la NATO kijeshi
18 Agosti 2023Matangazo
Duru hizo zimeliambia shirika la habari la Ujerumani, dpa, kwamba kuelekea maamuzi muhimu ya baraza la mawaziri, serikali imekiondoa kutoka kwenye rasimu ya sheria ya bajeti, kipengee kinachoitaka Ujerumani kutumia asilimia mbili ya pato lake jumla kwa ulinzi.
Mapema wiki hii, vyombo vyengine vya Ujerumani pia viliripoti taarifa hiyo.
Maazimio ya jumuiya ya NATO yanawataka wanachama wake wote kutumia kiwango hicho kwenye matumizi yake ya kijeshi ingawa Ujerumani na mataifa mengine ya Ulaya Magharibi hayajakifikia kiwango hicho.
Hivi majuzi, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema serikali yake itatumia kiwango hicho cha fedha katika kipindi cha muda mrefu.