Waganda wamejitokeza kwa wingi kusajiliwa katika jeshi la askari walinzi wa mitaa nchini Uganda ikiwa ni baada ya Rais Yoweri Kaguta Museveni kutoa agizo hilo hivi karibuni. Jeshi la akiba la wanajeshi 24,000 limebuniwa kwa nia ya kukabiliana na hali ya usalama inayoelezwa kuwa mbaya hasa maeneo ya mji mkuu Kampala.