1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Rwanda kufanyika Mwezi Julai mwakani

12 Desemba 2023

Rwanda itafanya uchaguzi wa rais na bunge mwezi Julai mwaka ujao. Rais Paul Kagame anatarajiwa kuomba kura zitakazomwezesha kuendelea kuiongoza nchi hiyo ya Afrika Mashariki ambayo ameitawala kwa miongo mitatu.

https://p.dw.com/p/4a5XE
Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul KagamePicha: Trinidad Express Newspaper/AFP

Amri kutoka ofisi ya rais imesema uchaguzi wa rais na wa wabunge 53 utafanyika tarehe 15 Julai na wabunge wengine 27 kutoka kwenye makundi maalum watateuliwa tarehe 16 Julai.

Kagame amekuwa rais wa Rwanda kuanzia mwaka 2000 lakini ameidhibiti nchi hiyo tangu jeshi lake la waasi lilipoingia mjini Kigali mnamo mwaka 1994 na kukomesha mauaji ya kimbari.

Soma pia:Mpango wa Sunak kuwapeleka wakimbizi Rwanda wapata upinzani

Mwezi Sptember aliiambia jarida la Jeune Afrique kwamba atawania tena urais akisema anajivuniaa kwamba wanyarwanda wana imani yeye.