Uchafuzi wa mazingira waharibu mfumo wa dunia kujiendesha.
31 Machi 2005Matangazo
Ripoti ya kina iliyotolewa inayohusu hali ya dunia yetu,imeonesha kuwa mwanadamu anaharibu mazingira katika kiwango kisichosemekana.Uchunguzi ulioendeshwa na wanasayansi 1,300 kutoka karibu nchi 100,umeonesha kuwa shughuli za binadamu zimesababisha kuchafuka kwa kiwango kikubwa mazingira ya dunia na hivyo mfumo wa kuviandalia dunia iliyobora vizazi vijavyo umo hatarini kutoweka.Mfumo wa dunia ambao upo hatarini kuangamia ni upande wa maji safi na viumbe vya baharini.
Imeelezwa na wanasayansi kuwa kiasi cha asilimia 60 ya mfumo wa dunia upo hatarini kuangamia.
Ingawa ripoti hiyo ya wanasaynsi imeonesha matumaini ya kuirekebisha hali hiyo iwapo sera za miongozo zitafuatwa,lakini hadi sasa hakuna kinachotekelezwa kukabiliana na mabadiliko haya.