1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UAE yashambulia wanamgambo Libya

Admin.WagnerD26 Agosti 2014

Maafisa wa Marekani wamsema ndege za kivita za Umoja wa Falme za Kiarabu zimefanya mashambulizi ya siri ambayo hayakutarajiwa kuyalenga maeneo ya wanamgambo wa Kiislamu nchini Libya.

https://p.dw.com/p/1D1EX
Libyen/ Kämpfe /Tripolis
Masambulizi mjini TripoliPicha: Reuters

Mzozo katika taifa hilo la Afrika ya Kaskazini unazidi kutokota wakati ambapo kundi hilo la wanamgambo wa Kiislamu likimteuwa waziri mkuu wao.

Awali jana maafisa wa Marekani walisema ndege hizo zilifanya mashambulizi mawali, dhidi ya wanamgambo hao ambao mjini Tripoli. Ndege hizo zinafanya mashambulizi kutoka Misri ambako, kumewekwa kambi.

Lengo la kutafuta ushawishi

Mashambulizi haya ya sasa katika mataifa ya kiarabu ambayo awali yalijikuta katika vita vya Libya yenyewe, Syria na Iraq yanaonesha kuwa na nia ya kuonesha mabavu na kutaka ushawishi. Kwa mara ya kwanza mashambulizi hayo yaliripotiwa na gazeti la Marekani-New York Times, na kikosi cha wanamgambo nchini Libya.

Libyen Kämpfe am Flughafen
Uwanjwa wa ndege wa TripoliPicha: Reuters

Afisa mmoja wa Marekani aliyezungumza pasipo kutaja jina lake aliliambia shirika la habari la Ufaransa pasipokutaja jina lake kuwa ndege za kivita za Umoja wa Falme za Kiarabu ndizo zilizofanya mashambulizi yote hayo. Maafisa wengine wawili vilevile wakadai Marekani haijashiriki na wala kusaidia chochote katika operesheni hiyo.

Marekani inajua lolote kuhusu mashambulizi?

Hata hivyo kwa pamoja maafisa hao hawakuthibitisha kama Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu imeiacha Marekani gizani kabisa kutokana na mashambulizi hayo.

Kwa mujibu New York Times shambulio la kwanza lilifanyika jumatatu ya wiki iliyopita, likilenga maeneo yanayodhibitiwa na wanamgambo wa Kiilsamu mjini Tripoli, yakiwemo maghala madodo ya silaha. Katika tukio hilo kumeelezwa watu sita kupoteza maisha.

Aidha gazeti hilo liliendelea kueleza kwamba duru ya pili ya shambulizi kama hilo ilifanyika mapema jumamosi, ikiwalenga wafyatua maroketi, magari ya jeshi na magahala mengine. Hata hivyo pamoja na madai hayo ya Marekani mpaka sasa Umoja wa Falme za Kiarabu haujasema chochote.

Kimsingi mashambuli hayo yanaelezwa kuwa na lengo la kuwadhibiti wanamgambo hao wasiweze kusonga mbele na kudhibiti uwanja wa ndege ambapo hata hivyo, hayakuzaa mtunda na hatimae wameweza kufanikiwa kukiweka katika himaya yao kiwanja hicho.

Umoja wa Falme za Kiarabu, ambayo imetumia mabilioni ya fedha zake katika kujihimarisha kijeshi kwa kununua ndege za kivita na zana nyingine za kisasa za kijeshi kutoka Marekani imeweza kuisadia Libya baadhi ya vifaa vyake na wataalamu wakati Misri imetoa eneo la kuwekwa kambi ya kijeshi katika kufanikisha operesheni zao.

Kimtazamo, Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri na Saudi Arabia zinatazama uwepo wa wangamgambo wa Kiislamu katika kanda hiyo kama kitisho kikubwa na wameunda umoja dhidi ya wanamgambo wao kwa kuita "hatari ya pamoja".

Operesheni hii ya sasa inafanyika baada ya chama cha wenye msimamo mkali wa Kiislamu GNC katika bunge la Lubya kuadhibu serikali ya Libya kwa kuchagua waziri mkuu na kuunda serikali hasimu.

Mwandishi: Sudi Mnette/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu