TOKYO: Mkataba wa mazingira waanza kutumika.
16 Februari 2005Matangazo
Mkataba juu ya kulinda mazingira uliopitishwa mjini Kyoto miaka saba iliyopita unaanza kutumika rasmi leo duniani kote.
Chini ya mkataba huo nchi za viwanda zimejiwajibisha kupunguza kwa asilimia 5 nukta 2 utoaji wa gesi
zinazoharibu mazingira hadi kufikia mwaka wa 2012.
Kuanza kutumika kwa mkataba huo wa Kyoto kumewezekana baada ya Urusi kutia saini pia.
Hata hivyo Marekani mpaka kufikia sasa bado inakataa kuidhinisha rasimu hiyo.
Mshindi wa nishani ya amani na mtetezi wa mazingira bibi Wangari Maathai wa Kenya alikuwa miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria ghafla ya kuzindua utekelezaji wa mkataba huo uliopitishwa miaka saba iliyopita mjini Kyoto.