Ingawa elimu ni haki ya msingi kwa binadamu, mara nyingi watu wanaoishi katika jamii zenye kipato cha chini huikosa. Mradi wa elimu wa Recycles Pay huko Lagos, Nigeria, unahakikisha kwamba watoto kutoka jamii hizi wanasalia shuleni huku wakikusanya taka za plastiki kama ada. Mpango huo unaruhusu wazazi au walezi kulipa karo za shule za watoto wao.