Tahadhari ya afya yatolewa Bangkok kufuatia uchafuzi wa hewa
9 Machi 2023Matangazo
Wizara ya afya ya umma imesema wilaya 50 za mji wa Bangkok jana zilirekodi viwango visivyo salama vya chembe hatari zinazoweza kuingia katika mishipa ya damu, vimesalia juu ya miongozo ya shirika la afya duniani WHO.
Changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa inaweza kudhibitiwa.
Kulingana na idara ya serikali ya kuthibti uchafuzi, viwango vya chembe hizo zinazojulikana kama PM2.5 vimekuwa juu ya viwango salama katika maeneo mengi ya Bangkok kwa muda wa siku tatu zilizopita.
Kriangkrai Namthaisong, daktari katika wizara hiyo, jana amewahimiza watoto na akina mama wajawazito kubaki majumbani, na kuwataka wale wenye ulazima wa kutoka nje kuvala barakoa ya N95 ya kukinga dhidi ya uchafuzi wa hewa.