Changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa inaweza kudhibitiwa.
4 Mei 2007Rajendra Pachauri mwenyekiti wa Umoja wa mtaifa katika jopo la kimataifa la mabadiliko ya hali ya hewa IPCC, amesema ripoti hiyo inaelezea kwa kina walimwengu kuhsu uzito wa suwala hili la mabadiliko ya hali ya hewa,atahri zake na jinsi wanavyoweza kupunguza utoaji wa gesi chafu kwa gharama ya chini.
Wataalamu hao wamesema kuimarisha matumizi ya nishati endelevu,kupunguza uharibifu wa misitu yetu ni baadhi ya mikakati inayotarajiwa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Ripoti hii ni ya tatu mwaka huu kutolewa na jopo hilo la kimataifa la IPPC na inatarajia pia kutoa gharama na manufaa ya baadhi ya sera zitakazohakikisha utekelezaji wa mikakati hii kwa mataifa mbalimbali.
Mwenyekiti huyo wa IPCC Rajendra Pachauri aliwaamibia waandishi habari kwamba jamii ulimwenguni lazima zitafute mbinu mpya za kupunguza matumizi viwanda vinayotoa gesi chafu.Kwani ikiwa utoaji wa gesi chafu utatiliwa maanani basi utapungua katika miongo miwili ijayo.
Kufikia sasa utoaji wa gesi chafu umeongezeka kwa silimia 70% tangu mwaka 1970,na utaongezeka kwa kati ya asilimia 25% hadi 90% katika miaka 25 ijayo. Ripoti hiyo inasema ongezeko hilo litatokana na kupanuliwa kwa matumizi ya nishati ya inayotengenezwa kutokana na vitu vilivyooza,nishati inayoonekana kutegemwa na na dunia katika siku zijazo.
Mapema wiki hii,katika mkutano huo wa mabadiliko ya hali ya hewa huko bankok,China amabyo imelaumiwa zaidi kwa utoaji mkubwa wa gesi chafu,ilijaribu kuviweka paembeni baadhi ya vipengele vya ripoti hiyo wanavyoviona vitazuia makuzi ya uchumi wake.
Wataalamu hao wameelezea matumaini yao,kwamba viongozi wameanza kutilia maanani ripoti hiyo ya IPPC kutokana na kuwa itapewa kipao mbele katika mazungumzo ya mataifa ya G8.
Ripoti hiyo iliyojadiliwa kwa siku tano na jopo hilo la mabadiliko ya hali ya hewa,inadhihirisha kwamba ikiwa mataifa yatawekeza katika teknologia ya kuzuia utoaji zaidi wa gesi chafu hivi sasa,watatumia chini ya asilimia 0.12 ya mapato yao tofauti na ikiwa hwatachukua hatua yeyote.
Baada ya mazungumzo haya ya IPPC Bangkok,mikutano miwili muhimu inayofuatia ya mabadiliko ya hali ya hewa itakuwa ile ya mataifa nane tajiri kwa viwanda,ya G8.Mwishoni wa mwaka huu,Mkutano wa kilele utafanyika Bali,kuweka malengo ya kupunguza utoaji wa gesi chafu.
Isabella Mwagodi