1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUfaransa

Sherehe za ufunguzi wa michezo ya Olimpiki zaibua utata

28 Julai 2024

Waandalizi wa Michezo ya Olimpiki mjini Paris wameomba radhi kwa kosa lolote wakati wa sherehe yao ya ufunguzi iliyozua utata, lakini wakakanusha kuwepo kwa nia yoyote ya kutoheshimu kundi lolote la kidini.­­­­­

https://p.dw.com/p/4ipyB
Wanariadha wa Ubelgiji wakati wa sherehe za ufunguzi za michezo ya Olimpiki ya 2024 mjini Paris, Ufaransa wakiwa kwenye boti katika mto Seine mnamo Julai 26,2024
Sherehe za ufunguzi za michezo ya Olimpiki ya 2024 mjini Paris, UfaransaPicha: Tingshu Wang/REUTERS

Baadhi ya makundi ya Kikatoliki na maaskofu wa Ufaransa wamelaani kile walichokiona kama "matukio ya kejeli dhidi ya Ukristo" katika gwaride la Ijumaa lililoandaliwa na muongozaji filamu Thomas Jolly.

Soma pia:Paris yanga'a katika sherehe ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki

Ukosoaji huo umelenga tukio linalohusisha wacheza densi, wanaume waliovalia kike ili kutumbuiza na mchezaji muziki wakiwa katika hali zilizoibua kumbukumbu za Alhamisi kuu, mlo wa mwisho unaosemekana Yesu alikula na mitume wake.

Hakukuwa na nia ya kutoheshimu kundi lolote la kidini

Msemaji wa michezo hiyo ya olmpiki ya mwaka 2024 Anne Descamps, amewaambia waandishi habari leo kwamba ni wazi hakukuwa na nia ya kutoheshimu kundi lolote la kidini.

Descamps ameongeza kusema ikiwa kuna watu waliokwazika, wanaomba radhi.