SiasaUholanzi
Sera ya Uhamiaji yaiangusha serikali ya Uholanzi
8 Julai 2023Matangazo
Rutte amesema tofauti zilizojitokeza kuhusu sera hiyo baina ya vyama washirika haziwezi kurekebishwa na kwamba uamuzi wa kuivunja serikali ulikuwa wa lazima. Hii leo Rutte amepangiwa kuwa na mkutano na Mfalme Willem-Alexander kumwarifu rasmi uamuzi wake wa kujiuzulu na inatarajiwa uchaguzi mpya utaandaliwa mwezi Novemba.
Chanzo cha mvutano ni pendekezo la chama cha Rutte cha VVD kinachoegemea siasa za mrengo wa kulia la kutaka kuzuia wahamiaji walio nchini Uholanzi kujiunga na familia zao.
Pendekezo hilo linapingwa vikali na chama cha kihafidhina cha Christian Unioni kinachotaka uwepo uwezekano wa kuwaruhusu watoto wa wakimbizi wa vita kujiunga na wazazi wao nchini Uholanzi.