1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda kufanya uchaguzi wa rais na wabunge kwa pamoja

Angela Mdungu
25 Machi 2023

Baraza la mawaziri la Rwanda limesema kupitia ofisi ya waziri mkuu kwamba limeamua kuoanisha tarehe za uchaguzi wa rais na wabunge nchini humo

https://p.dw.com/p/4PF1n
Ruanda | Emmanuel Macron in Kigali | Paul Kagame
Picha: Jean Bizimana/REUTERS

Katika mkutano wa baraza hilo ulioongozwa na Rais Paul Kagame, mawaziri walipitisha pendekezo lake la kurekebisha katiba ili kuruhusu kufanyika pamoja kwa chaguzi hizo.

Uchaguzi mkuuwa taifa hilo, sasa unatarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu, ambapo awali ulipangwa kufanyika uchaguzi wa rais pekee. Kufanya hivyo kungechelewesha uchaguzi wa wabunge hadi mwezi Septemba mwaka huu. Hatua hiyo inayosubiri kupitishwa na bunge ilitangazwa sambamba na ile ya kuachiliwa huru kwa mkosoaji wa Rais Kagame, Paul Rusesabagina aliyekuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa makosa ya Ugaidi.

Chanzo: AFPE