SiasaMali
OHCHR: Jeshi la Mali na wanajeshi wa kigeni wameuwa watu 500
12 Mei 2023Matangazo
Hayo yameelezwa katika ripoti iliyochapishwa leo na tume ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, OHCHR. Tume hiyo imesema inaamini kwamba mauaji hayo yaliyotokea katika mji wa Moura yalifanywa kwa njia za ukiukaji sheria na misingi ya sheria ya kimataifa. Waliouwawa ni pamoja na wanawake 20 na watoto 7. Ripoti ya uchunguzi uliofanywa na kitengo kinachoshughulikia haki za binadamu katika ujumbe wa kulinda amani Mali, Minusma, imebaini kwamba jeshi la Mali na wanajeshi wa kigeni waliokuwa wamemaliza shughuli zao za doria katika eneo hilo ndio walioendesha mauaji hayo. Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema yaliyobainishwa kwenye ripoti hiyo yanatisha.