1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Walinda amani wawili wa UN wajeruhiwa katika mripuko Mali

19 Aprili 2023

Umoja wa Mataifa umesema askari wake wawili wa kulinda amani walijeruhiwa baada ya kuripukiwa na bomu la kutegwa ardhini katikati mwa Mali

https://p.dw.com/p/4QIBT
Mali | Bundeswehrsoldaten in der UN-Base in Gao
Picha: Adrian Wyld/The Canadian Press/picture alliance

Taarifa ya umoja huo imeongeza kuwa mripuko huo umetokea karibu ya kijiji cha Amba, ukilenga msafara wa walinzi wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukielekea katika mji huo. Taarifa hiyo haikueleza juu ya uraia wa askari waliojeruhiwa.

Kijiji cha Amba kiko umbali wa kilomita zipatazo 75 magharibi mwa mji wa Douentza katika mkoa wa Mopti.

Ijumaa iliyopita askari mwingine wa ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA alijeruhiwa vibaya baada ya gari alilosafiria kukanyaga bomu jingine la kutegwa ardhini. Gari hilo lilikuwa likisafiri kutoka mji wa kali wa Timbuktu.