1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiKenya

Ripoti: Watoto katika baadhi ya kaunti Kenya wapo hatarini

8 Novemba 2023

Watoto katika kaunti za Nairobi,Kiambu na Nakuru wako kwenye hatari kubwa ya kufanyiwa madhila ikilinganishwa na kwengine.

https://p.dw.com/p/4YZ49
Rais wa Kenya Willium Ruto
Rais wa Kenya Willium RutoPicha: DW

Visa hinavyoripotiwa zaidi ni unajisi na ubakaji. Kaunti ya Nandi ndiyo salama zaidi kwa watoto inafafanua ripoti mpya ya baraza la Taifa la utekelezaji wa haki, NCAJ. Uhalifu pia umeongezeka katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Kulingana na ripoti mpya ya baraza la Taifa la utekelezaji wa haki, NCAJ, asilimia 25 ya watu waliochukuliwa hatua za kisheria kwa kipindi cha mwaka 2022/23 walishtakiwa kwa mapigano na kuvuruga Amani ya jamii. Idadi hiyo imeongezeka kwa zaidi ya 1000 katika kipindi hicho.

Idadi ya Waliokamatwa kwa uvamizi wa kimwili, ulawiti, unajisi na ubakaji  ilifikia 7259. Kulingana na ripoti hiyo, Visa vya unajisi ndio vingi zaidi ambavyo ni 78% nao ubakaji ni 12%.

Tathmini hiyo imebainisha kuwa kaunti za  Nairobi, Kiambu na Nakuru ndio maeneo hatari zaidi kwa watoto kupata madhila kadha wa kadha.

Soma pia:Watoto 4 wafa, 15 wajeruhiwa kwa kuangukiwa na kanisa Burundi

Idadi ya Visa vya kuwadhulumu watoto imeripotiwa kuwa 23,261 kaunti ya Nairobi,12,271 Kiambu na Nakuru imefikia 10,457.

Kwa jumla watoto 188,760 wanaripotiwa kupitia madhila aina mbalimbali katika kipindi hicho.

Kaunti ya Nandi iliyo ripoti Visa 517 vya madhila ndio salama zaidi kwa watoto inaeleza ripoti ya baraza la Taifa la utekelezaji wa haki.

Kwa upande wake, kaunti ya Kakamega ni ya kwanza kuwahi kutoa huduma za uwakilishi mahakamani pasina malipo kwa wahanga wa dhulma za kijinsia aghalabu watoto.

Rose Muhanda ni afisa wa matibabu katika kaunti ya Kakamega na anasisitiza kuwa mpango huo mpya umeleta tija tangu kuzinduliwa.

Matumizi ya mihadarati yaongezeka

Utafiti huo pia umebaini kuwa kaunti za Muranga , Nakuru (276) na Kericho (182) ndizo zilizo na idadi kubwa zaidi ya watoto watundu.

Mahakama ya Juu Kenya
Mahakama ya Juu KenyaPicha: Yasuyoshi Chiba/AFP

Watoto walio na maadili mazuri zaidi ni wa kutokea kaunti za Tana River, Uasin Gishu, Wajir, Vihiga, Turkana, Trans Nzoia na Laikipia.

Viviane Mbaka ni afisa mtendaji wa masuala ya sheria katika kaunti ya Kalamega na anaelezea umuhimu wa kuwalinda watoto kisheria.

Takwimu za utafiti huo mpya zinaeleza pia kuwa matumizi ya mihadarati na dawa za kulevya yameongezeka kwa 2000 katika kipindi cha mwaka uliopita kutokea visa 8077.

Soma pia:Ongezeko la mfumuko lamaanisha njaa kwa watoto- uchunguzi

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa baraza la Taifa la utekelezaji wa haki NCAJ, Jaji Mkuu Martha Koome, uhalifu kwa jumla umeongezeka kutokea Visa 85,539 mwaka 2020/22 hadi 97,301 mwaka 2022/23.

Wengi ya wanaozuiliwa jelakwa uhalifu  wamenyimwa nafasi ya kuachiliwa kwa dhamana au  kushindwa kuilipa. 

Usafirishaji haramu wa binaadamu watishia watoto wa Afrika