Rasimu mpya ya ufadhili wa tabianchi yazusha mgawanyiko
23 Novemba 2024Ilipendekeza ufadhili wa dola bilioni 250 kwa mwaka ifikapo 2035 kutoka kwa nchi tajiri kuelekea nchi maskini. Kiasi hicho cha fedha kinaziridhisha nchi zitakazokuwa zikizitoa, lakini sio zile zitakazokuwa zikipokea.
Soma pia:Azerbaijan kutoa pendekezo jipya la ufadhili wa tabianchi
Ni zaidi ya mara mbili ya lengo la awali la dola bilioni 100 kwa mwaka lililowekwa miaka 15 iliyopita, lakini chini ya robo ya kiasi kilichoombwa na mataifa yanayoendelea ambayo yameathiriwa zaidi na hali mbaya ya hewa.
Lakini mataifa tajiri yanasema kiasi hicho kinafaa na kinafikia ukomo wa wanachoweza kutoa. Pendekezo hilo halijaziridhisha nchi zinazoendelea, ambazo zinaona mikutano kama hii kama tumaini lao kubwa kuyashinikiza mataifa tajiri kwa sababu wao sio sehemu ya mikutano inayofanywa na nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani. Mkutano huo wa wiki mbili wa mazingira ulitarajiwa kukamilika Ijumaa mjini Baku, Azerbaijan lakini uliingia katika muda wa ziada na unatarajiwa kendelea hadi Jumamosi.