1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

A.Kusini kuanza uchunguzi wa tuhuma za silaha

28 Mei 2023

Rais wa Afrika ya Kusini, Cyril Ramaphosa ameteua jopo la kuchunguza tuhuma zilizotolewa na Marekani kuwa meli ya Urusi ilisafirisha silaha kutoka katika kambi ya jeshi la wanamaji karibu na Cape Town mwaka uliopita.

https://p.dw.com/p/4Rv0G
South Africa Arms To Russia I The Russian vessel Lady R
Picha: AP/picture alliance

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ikulu ya Afrika ya kusini mapema leo. Awali, Mei 11, balozi wa Marekani nchini humo Reuben Brigety alisema kuwa ana uhakika kwamba meli moja ya Urusi iliyotia nanga katika kambi ya jeshi la wanamaji mjini Simons, Cape town ilikusanya silaha kutoka Afrika Kusini kuelekea nje ya nchi.

Afrika ya Kusini, imekuwa ikikanusha madai hayo na kusema kuwa haiegemei upande wowote katika vita nchini Ukraine.

Tuhuma hizo zimesababisha mvutano wa kidiplomasia kati ya Afrika Kusini na Urusi na kuzua maswali juu ya nafasi ya Pretoria katika mzozo wa Ukraine.