SiasaAfrika Kusini
Afrika Kusini na madai ya Marekani kuiuzia Urusi silaha
13 Mei 2023Matangazo
Siku ya Alhamisi, Balozi Reuben Brigety alidai kuwa silaha zilipakiwa kwenye meli ya Urusi iliyotia nanga katika eneo la kikosi cha jeshi la majini cha Afrika Kusini cha Simonstown mwezi Desemba.
Afrika Kusini imesema haina rekodi ya kuidhinisha mauzo ya silaha na Rais Cyril Ramphosa ameamuru uchunguzi ufanyike na utaongozwa na jaji mstaafu.
Serikali ya Afrika Kusini imesema imesikitishwa na hatua ya Brigety kutoa madai hayo hadharani na sio kufuata utaratibu wa kidiplomasia.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Naledi Pandor amelizungumzia suala hilo na waziri mwenzake wa Marekani, Antony Blinken.