1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramaphosa asafishwa makosa ya kulipotosha bunge

10 Machi 2020

Mahakama kuu Afrika Kusini imemsafisha rais Cyril Ramaphosa kuhusiana na mashtaka ya kulidanganya bunge kuhusu chanzo cha michango ya kifedha kwenye kampeni yake ya mwaka 2017 kukiongoza chama tawala ANC.

https://p.dw.com/p/3Z8pi
Südafrika Präsident Cyril Ramaphosa
Picha: AFP/M. Spatari

Uamuzi huo umeiweka kando ripoti iliyokuwa na uwezekano wa kumharibia rais huyo, iliyotolewa na taasisi ya kupambana na rushwa.

Mlinzi wa umma Busssiwe Mkhwebane alidai mwezi Julai kwamba Ramaphosa alilipotosha kwa maksudi bunge kuhusu mchango wa rand laki tano  ambazo ni sawa na dola za Marekani elfu 32 na mia 5 katika kampeni yake ya kumrithi Jacob Zuma kama mwenyekiti wa chama cha ANC.

Mahakama kuu ya Pretoria imetupilia mbali ripoti ya mlinzi wa mali za umma iliyomshutumu rais Ramaphosa kudanganya bunge kwa makusudi  kuhusu mchango wa kampeni wa dola 34,000 uliotolewa na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Africa Global Operations awali ikijulikana kama Bosasa. 

Hatua hii inaonekana kuongeza nguvu kisiasa ya rais huyo wa Afrika Kusini aliyeapa kupambana na suala la ufisadi nchini humo. 

Ramaphosa alichukua nafasi ya Jacob Zuma kama mwenyekiti wa chama tawala ANC naa baadae kama rais baada ya Zuma kujiuzulu kufuatia shinikizo kutokana na madai kadhaa ya ufisadi.