1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Macky Sall awasamehe wafungwa wa kisiasa

27 Februari 2024

Rais wa Senegal Macky Sall, amependekeza muswada wa sheria ambao utatoa msamaha kwa waandamanaji wa kisiasa waliokamatwa kati ya mwaka 2021 na 2024.

https://p.dw.com/p/4cvRb

Sall amependekeza hilo huku akiongoza mazungumzo ya siku mbili ya kujaribu kumaliza mgogoro nchini humo uliotokana na hatua yake ya kuahirisha uchaguzi mkuu.

Macky Sall ambaye muhula wake wa pili madarakani unakamilika rasmi Aprili 2, alitangaza pendekezo hilo katika ufunguzi wa kile alichokiita "mazungumzo ya kitaifa" ambayo pia yanalenga kuweka tarehe mpya ya uchaguzi.

Soma pia: Umoja wa Ulaya waitaka Senegal kutoa hakikisho la uhuru wa kimsingi

Kulingana na makundi ya kutetea haki za binaadamu, zaidi ya watu 1,000 wamekamatwa tangu mwaka 2021 wakati wa vurugu za kung'ang'ania madaraka kati ya Sall na kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko.

Taifa hilo la Afrika Magharibi linakabiliwa na mzozo mbaya zaidi wa kisiasa kuwahi kutokea kwa miongo kadhaa, baada ya Sall ghafla kuahirisha ghafla uchaguzi saa kadhaa kabla ya kampeni za uchaguzi huo kuanza rasmi. Uchaguzi wa Senegal ulikuwa ufanyike Februari 25.