1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Nigeria atoa wito wa kusitishwa maandamano

4 Agosti 2024

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu ametoa wito wa kusitishwa kwa maandamano ya nchi nzima na kukomesha "umwagaji damu" ikiwa ni baada ya vikosi vya usalama kukabiliana na maandamano ya kupinga hali ngumu ya kiuchumi.

https://p.dw.com/p/4j5bd
Maandamano ya Nigeria
Vikosi vya usalama vya Nigeria vikirusha gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wakati wa maandamano Agosti 1, 2024.Picha: Kola Sulaimon/AFP

Katika hotuba kupita televisheni, Tinubu amewataka waandamanaji  kusimamisha maandamano mengine yoyote na kutoa nafasi ya mazungumzo, ikiwa ni kauli yake ya mwanzo kwa umma tangu maandamano yalipoanza Alhamisi.

Katika hotuba hiyo alionesha kuwa amesikia kilio cha wananchi, kuelewa machungu waliyonayo na mfadhaiko uliosababisha waandamane na hivyo kutoa ahadi ya serikali kushughulikia kero zao.

Juma lililopita maelfu ya waandamanaji walianza kuingia barabarani kupinga sera za serikali na gharama kubwa ya maisha. Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeshutumu vikosi vya usalama kwa kuwaua takriban waandamanaji 13, huku polisi wakisema watu saba tu ndio waliofariki na kukana kuhusika na mauaji hayo.