Duda: Poland iko tayari kupokea silaha za nyuklia za NATO
23 Aprili 2024Matangazo
Rais Duda amesema yuko tayari ikiwa washirika hao watachukua uamuzi kama huo kwa lengo la kuimarisha usalama katika eneo la Mashariki la Muungano huo wa kijeshi.
Hata hivyo, Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk amesema anahitaji kupata taarifa zaidi juu ya mazingira yayoliyopelekea rais Duda kutoa kauli ambayo amesema ni kubwa na nzito mno. Tusk amesisitiza kuwa mipango yoyote ni lazima iratibiwe kikamilifu na kuhakikisha ikiwa ni uamuzi wa wote.
Mwaka jana, Urusi ilituma makombora ya kimkakati ya nyuklia huko Belarus huku kukiwa na hali ya mvutano kati yake na NATO kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine. Poland, ambayo inapakana na Ukraine upande wa magharibi, inachukuliwa kuwa mshirika muhimu wa Kiev katika vita hivyo.