1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tusk aonya kuwa Ulaya imeingia "enzi za kabla ya vita"

Sylvia Mwehozi
30 Machi 2024

Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk ameonya juu ya kitisho cha migogoro inayoikabili Ulaya, akisema kuwa kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia, Ulaya imeingia katika "enzi ya kabla ya vita."

https://p.dw.com/p/4eGti
Poland | Donald Tusk
Waziri Mkuu wa Poland Donald TuskPicha: Omar Marques/Getty Images

Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk ameonya juu ya kitisho cha migogoro inayoikabili Ulaya, akisema kuwa kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia, Ulaya imeingia katika "enzi ya kabla ya vita."

Katika mahojiano yake na shirika la vyombo vya habari la Ulaya LENA, Tusk alisema kuwa vita sio tena dhana iliyopita bali ni halisi na vimeanza zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Kiongozi huyo ameeleza kuwa kinachotia mashaka zaidi kwa hivi sasa ni kwamba hali yoyote inawezekana, akionya kizazi cha sasa kuwa kinapaswa kuzoea ukweli kwamba Ulaya imeingia enzi mpya za kabla ya vita.

Tusk ambaye ni rais wa zamani wa Tume ya Ulaya, ambaye nchi yake imekuwa ikiunga mkono Ukraine, amesisitiza kuwa kama Kyiv itashindwa hakuna hata mmoja Ulaya atakayekuwa salama.