JamiiJamhuri ya Afrika ya Kati
Raia wa China wauawa Jamhuri ya Afrika ya Kati
20 Machi 2023Matangazo
Taarifa iliyotolewa jana Jumapili na Meya wa Bambari, Abel Matchipata imeeleza kuwa watu wengine wawili wamejeruhiwa. Meya huyo amesema wahanga ni wafanyakazi wa Kichina katika mgodi wa dhahabu wa Chimbolo, unaoendeshwa na kampuni ya Gold Coast Group.
Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulizi hilo, lakini kundi la waasi linalojulikana kama Muungano wa Wazalendo kwa ajili ya Mabadiliko, CPC ndiyo linashukiwa kuhusika.
Kundi hilo limekuwa likiendesha mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya majeshi ya serikali. Kundi hilo lina mafungamano na Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Francois Bozize.